Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa taasisi, vyuo vya afya, na waganga wafawidhi kuhakikisha wanawafuatilia kwa karibu wataaluma wa afya walio katika mafunzo kwa vitendo ,(interns) kupata umahiri, utalaamu, na maadili yakazi.
Ameyabainisha hayo wakati akiongea na wasajili wa Mabaraza ya kitaaluma yaliyopo chini ya wizara afya katika ukumbi wa wizara jijini Dodoma, amesema ni vema kwa interns kufanya mitihani baada ya mafunzo, pia amewahasa mabaraza kuharakisha utaratibu huo.
Aidha ametoa wito kwa hospitali zote zinazotoa mafunzo yasiyostahili na kusababisha interns kumaliza mafunzo bila umahiri
“Serikali imeanza kuchunguza hizo hospitali na kama hazitasimamia vyema hawa wanataaluma walio mafunzoni, tutazifutia kibali cha kuwapokea”. Amesema Profesa Abel.
Sambamba na hilo Profesa Makubi amewahasa wanafunzi walio kwenye mafunzo kwa vitendo kujituma katika mafunzo yao, kuonyesha nia ya kujifunza na kuweka bidii katika mafunzo yao ya vitendo mahali walipo.