Mabingwa wa kihistoria  wa Tanzania Yanga sc imeibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya wakata miwa wa Kagera sugar .

Shukrani za dhati kwa mchezaji toka nchini DRC MukokoTonombe  ambae dakika ya 71 alipeleka kilio kwa wapinzani wao Kagera sukari .

Yanga  imefanikiwa kupata ushindi wao wapili mfululizo katika ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kuifunga timu ya Kagera sugar mchezo uliopigwa dimba la kaitaba mjini bukoba

Nahodha wa Yanga Deus kaseke amesema wamecheza na timu nzuri na timu hiyo ilikosa Bahati huku wao wakitumia nafasi waliyopata.

Ushindi huo ni wa sita mfululizo kwa Yanga dhidi ya Kagera katika Uwanja wa Kaitaba kama ambavyo reodi zinavyoonyesha tangu msimu wa 2015/16.

Yanga sc sasa inaongoza ligi baada ya kufikisha jumla ya pointi 7 baada ya kushuka dimbani mara 3 huku wakitarajia kucheza wiki ijayo dhidi ya Mtibwa sugar katika dimba Jamhuri Mjini Morogoro.

ZEC yawaengua wagombea 15
Prof. Makubi: hakuna kuhitimu mafunzo kwa vitendo bila mtihani