Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa umahiri, weledi na ubunifu, ili malengo ya sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaweze kufikiwa.

Prof. Nombo ametoa wito huo hii leo Februari 28, 2023 Jijini Dodoma wakati wa mapokezi na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula baada ya kuteuliwa na  Rais Dkt. Samia ambapo amesema Wizara hiyo imepewa jukumu kubwa la kuhakikisha elimu bora inatolewa nchini na kuimarisha Sekta ya Sayansi na Teknolojia.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo.

Amesema, Wizara ipo katika hatua za mwisho za kuhuisha sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na Mitaala, huku akisisitiza kuwa si Tanzania pekee inayofanya mageuzi hayo bali kwasasa Dunia ipo katika mageuzi ya kielimu.

“Mageuzi katika utendaji kwa kufanya kazi kwa weledi, umahiri, ubunifu na uwazi ni muhimu ili kufikia yale mageuzi tunayoyatamani katika sekta ya elimu,” amesisitiza Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Franklin Rwezimula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kutumikia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi na kuendelea kuboresha sekta ya elimu.

Ushirikiano huleta ufanisi wa kazi: Dkt. Yonazi
Safari za ndege Tanzania, Saudi Arabia mbioni