Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imewaachia huru washtakiwa wote saba ambao ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, baada ya mahakama hiyo kusema kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri una utata na hivyo Mahakama kushindwa kuthibitisha makosa hayo.
Hii ni mara ya pili ambayo Lengai Ole Sabaya anashinda dhidi ya Jamhuri baada ya awali kushinda rufaa ya kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 ambayo ilitolewa Mei 06, 2022 ambapo kwenye rufaa hiyo Sabaya alikuwa pamoja na wenzake wawili, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.
Hata hivyo Sabaya ataendelea kubaki rumande kutokana na kukabiliwa na kesi nyingine mkoani Kimanjaro.