Mwanamume mmoja amezirai na kuaga dunia papo hapo wakati akifanya mazoezi katika ukumbi wa mazoezi eneo la Koinange jijini Nairobi.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 51 alikimbizwa hospitali moja iliyokuwa karibu lakini akaripotiwa kuwa amefariki tayari.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, mwanaume huyo ni mzoefu wa kufanya mazoezi katika ukumbi huo kwa muda na tatizo hili lilitokea alipokuwa akifanya mazoezi kwenye mashine ya kukimbia.

Polisi wamesema kuwa wanapanga kuufanyia mwili huo upasuaji ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Katika hatua nyingine mwanamke mmoja amepatikana akiwa amefariki baada ya siku kadhaa za kufunga na kuomba mtaani Embakasi Kaunti ya Nairobi.

Mwili wa Catherine Kibara mwenye umri wa miaka 78 ulipatikana katika kitanda chake baada kutookena kwa siku kadhaa.

Polisi wanahisi Catherine alifariki kutokana na njaa kwa sababu aliishi pekee yake na hakuwa na mazoea ya kukosa kupokea simu.

Sabaya aachiwa huru
Watu 19 wamefariki kwa ajali ya Costa