Watu 19 wamefariki dunia baada ya basi dogo aina ya Costa kugongana uso kwa uso na lori la mizigo karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkiani Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi akiongea kwa njia ya simu na Dar 24, amethibitisha kutokea vifo hivyo na kusema kwa sasa majeruhi wanaendelea kutibiwa hospitali.

“Ajali imetokea katika mazingira ya Costa kugonga Lori lililokuwa limeharibika ambapo inaonekana dereva alikua amechoka na alikua mwendokasi,” amesema Kamanda Bukumbi.

Kamanda Bukumbi ameongeza kuwa, “baada ya ajali hiyo ya kwanza kutokea wakati jitihada za kuokoa majeruhi zikiendelea lilitokea lori jingine na kugonga ile costa ya kwanza hivyo kuwa na ajali mbili kwa wakati mmoja.”

Ameongeza kuwa sababu za ajali ni mwendokasi wa dereva wa Costa, ambao ulichangiwa na uchovu aliokuwa nao kwa sababu ya kusafiri usiku kucha kutuka Dar es Salaam hivyo kupungruza umakini barabarani.

Watu waliokuwa katika eneo la tukio wamesema jitihada za kuokoa majeruhi na kutoa miili ya watu ziliendelea kwa muda mrefu.

Taarifa zinasema eneo ambalo ajali hiyo imetokea, ndilo ambalo basi la Majinja liliangukiwa na lori mwaka 2015 na kuua zaidi ya watu 40.

Mwanaume afariki 'Gym'
Simba SC yashindwa kumsajili Victorien Adebayor