Mfuko wa pensheni Kwa watumishi wa umma – PSSSF ,imeshiriki katika kutoa elimu juu ya huduma ya kiganjani Kwa lengo la kurahisisha na kuwafikia Wanachama pamoja na wastaafu kuweza kuwafikia huduma hiyo.

Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma – PSSSF, Vonnes Koka ameyasema hayo wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana, Kitaifa ambayo yanafanyika katika kiwanja cha stendi ya zamani mjini Babati, Mkoa Manyara.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Donald Maeda amesema katika Banda la PSSSF mwanachama atapata huduma zote za Mfuko zinazopatikana katika ofisi zote za Mfuko.

Huduma hizo, ni kupata taarifa za michango yake, kupata taarifa za mafao mbalimbli, Uhakiki wa Wastaafu pamoja na Elimu kwa Wanachama, pia Wanachama na Wastaafu wataunganishwa na PSSSF Kiganjani.

Robertinho: Ninamrudisha rasmi Aishi Manula
Wright: Bila Ivan Toney hakuna ubingwa Arsenal