Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma – PSSSF, umetaja sababu ya kupokea tuzo toka kwa Taasisi ya Kimataifa ya Hifadhi ya Jamii (International Social Security Association-ISSA) kuwa inatokana na jinsi Mfuko ulivyoweza kupunguza gharama za uendeshaji na ulipaji wa mafao kwa wakati.

Akizungumzia tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema sababu nyingine
iliyoifanya ISSA kutoa tuzo kwa Mfuko huo ni pamoja na mafanikio iliyoyapata katika kipindi kifupi baada ya kuunganishwa kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, GEPF NA LAPF na kuwa PSSSF.

Amesema, “kwenye suala la kuunganisha mifuko yapo mambo manne ambayo ISSA imeyaona na kuona ni mafanikio ambayo ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji, kutoa mafao yanayofanana kwa wanachama wa Mfuko licha ya kutoka kwenye mifuko tofauti, kukabiliana na madeni kabla ya mifuko kuunganishwa na pia suala la uwekezaji hususan katika viwanda.”

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),  Dkt. Aggrey Mlimuka (kulia) akipokea tuzo ya Kimataifa inayotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Hifadhi ya Jamii (International Social Security Association-ISSA) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba.

Aidha, Kashimba aliishukuru Bodi ya Wadhamini kwa usimamizi mzuri na hivyo kuufanya Mfuko huo kufanya vizuri na kusema, “duniani wanasema karibu asilimia 85 ya kampuni zilizoungana huwa zinashindwa, lakini muunganiko wetu sisi umeendelea kufanya vizuri hadi kuivutia taasisi hii kubwa kuifanya PSSSF kuwa mfano wa kuigwa.”

Awali, Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbarouk Magawa alidokeza kuwa eneo lingine ambalo liliwavutia watoa tuzo ni jinsi mfukoulivyofanya maboresho makubwa katika utoaji wa huduma kwa wastaafu na wanachama na kuzungumzia Huduma kwa wananchama, jinsi wanavyokusanya michango, kulipa mafao, kutoka kwenye matumizi ya hundi kulipa mafao, wanavyohakiki wastaafu.

Chelsea yamtega Mauricio Pochettino
Bosi Leicester City awajibu waliomtusi