Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar inatarajia kupokea timu ya wataalamu na Wawekezaji kutoka Qatar.

Dkt. ameyasema hayo hii leo Mei 30 2023 katika mkutano wake wa kila mwisho wa Mwezi na Waandishi wa Habari uliofanyika Ikulu, Zanzibar wakati akizungumzia ziara yake hivi karibuni ya nchi hiyo.

Amesema, katika ziara hiyo pia alipata fursa ya kueleza maeneo ya uwekezaji na biashara yanayopatikana Zanzibar katika ziara hiyo alipokutana na Wawekezaji Nchini humo.

Aidha Dkt. Mwinyi amezungumzia sera ya Uchumi wa Buluu ikiwemo Mafuta na Gesi , Uvuvi, Bandari , usindikaji wa bidhaa za bahari na fursa zinazopatikana katika maeneo ya sekta ya utalii ikiwemo wa fukwe, mambo ya Kale na utalii wa kisasa wa kumbi za Mikutano ya Kimataifa.

Mauricio Pochettino aonywa mapema Chelsea
Kocha Nasreddine Nabi aishtukia USMA