Bosi wa Leicester City, Aiyawatt Srivaddhanaprabha, ametoa kauli ya kishujaa akisema kuwa timu itarejea tena Premier League hivi karibuni.

Aiyawatt amesema amepokea jumbe nyingi za kejeli na matusi kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wamechukizwa na kitendo cha klabu yao kushindwa kubaki Ligi Kuu ya England.

Familia yake imekuwa ikiimiliki Foxes tangu 2010, na Aiyawatt akichukua jukumu mnamo 2018 baada ya kifo cha baba yake Vichai, wakati huo, wamepandishwa daraja, wakashinda Ligi Kuu na Kombe la FA.

“Kushuka daraja bila shaka ni kikwazo kikubwa,” mwenyekiti huyo alisema katika taarifa yake.

“Tunapata hasara na maumivu ya kushushwa daraja kwa pamoja. Lakini tutarudi,” alisema Srivaddhanaprabha.

Wachezaji kadhaa nyota wa Leicester, akiwemo Youri Tielemans, Jonny Evans na Caglar Soyuncu pamoja na meneja Smith, ambaye alichukua nafasi ya Brendan Rodgers aliyetimuliwa zikiwa zimesalia mechi nane wanatarajia kuondoka klabuni hapo kwa kuwa mikataba yao inafikia ukingoni.

Sababu PSSSF kupewa tuzo Kimataifa zatajwa
Ziara za Rais Dkt. Samia, Viongozi nje ya nchi zimezaa matunda