Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo ndio Mratibu wa ushirikiano na
uhusiano baina ya Tanzania na nchi nyingine duniani katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii
imesema kuwa, ziara za viongozi wetu wa kitaifa nje ya nchi zimeliletea taifa mafanikio makubwa ya
kiuchumi na kijamii.

Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Stergomena Tax ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24.

“Ziara hizi za Rais Dkt. Samia na Viongozi wengine zimeimarisha uhusiano wa Kimataifa na nchi rafiki, Jumuiya za Kikanda, Jumuiya za Kimataifa na kuleta mafanikio kiuchumi na kijamii, kufungua masoko, ongezeko la watalii, upatikanaji wa misaada na mikopo yenye masharti nafuu kwa miradi mbalimbali katika sekta za kijamii na kiuchumi,” amefafanua Dkt. Stergomena.

Ziara ya Rais Dkt. Samia aliyoifanya nchini nchini Misri Novemba 11, 2021.

Ameyataja mafanikio ya ziara hizo kuwa ni pamoja na Sheikh Tamim Bin Hamad Al Thani, Amiri na Mtawala wa Dola ya Qatar kuahidi kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa masomo ya afya, kujenga jengo la mama na mtoto na kuleta wataalamu wa afya nchini kwa lengo la kubadilishana ujuzi.

Mengine ni ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari na kusaidia baadhi ya miradi ya kimkakati ya maendeleo ya Tanzania kupitia mfuko wa Maendeleo wa Qatar, Tanzania na Oman kusaini hati za makubaliano ya ushirikiano katika sekta za elimu ya juu na mafunzo ya ufundi, utunzaji wa nyaraka na ujenzi wa kituo cha uhifadhi wa taarifa.

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(katikati) akiwa mahojiano na kituo cha runinga cha “Chinese Satelite Travel”

Mafanikio mengine ni Tanzania na China kusaini Hati ya Makubaliano kuruhusu zao la parachichi kuingia katika soko la China na Hati ya Makubaliano kuruhusu mazao ya uvuvi yakiwemo mabondo ya samaki kutoka Tanzania kuingia katika soko la China.

China kuipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 297.64 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa mawasiliano vijijini, msaada wa Dola za Marekani milioni 24.86 kwa ajili ya upanuzi wa JKCI na mkopo wa Dola za Marekani milioni 58.3 kwa ajili ya kugharamia upanuzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume Zanzibar.

Bosi Leicester City awajibu waliomtusi
Azam FC yaitibulia Simba SC usajili 2023/24