Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ndani ya miezi 12 mpaka 18 utekelezaji wa umeme wa jua na umeme wa upepo utaanza kwa haraka kwani wanatarajia ndani ya mwaka mmoja umeme huo uwe unatumika.

Makamba amesema, “jana tumesaini mkataba wa kuingiza umeme wa jua kwenye gridi kwa mara ya kwanza. Na sasa hivi ukitazama mchanganyiko wa vyanzo kwenye gridi yetu, utaona sasa maji yako chini, gesi ndio inaongoza (65%) na 30% ni maji. Kwa hiyo tayari tunapunguza utegemezi (wa maji).”

‘Tumekua tukitegemea maji kuzalisha umeme, tumekua na taabu maji yakikauka. Tunachofanya sasa hivi ni kuongeza vyanzo vya umeme ili kuepukana na risk inayoweza kujitokeza,” amesema Waziri Makamba.

Ziara ya CCM yampa Balozi wa shina nyumba ya kuishi
Wastaafu wataka teknolojia itumike uhakiki mifuko ya hifadhi