Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameamuru kuongezwa kwa ukubwa la ukubwa wa vikosi vya jeshi la nchi hiyo, hatua ambayo inaashiria kuwa ni maandalizi ya kukabiliana na upungufu wa wanajeshi wa kujitolea kwa muda mrefu kwenye vita vya Ukraine.
Putin, amepandisha idadi inayolengwa ya wahudumu wa huduma hai kkutoka wanajeshi 137,000, hadi kufikia wanajeshi milioni 1.15, wanaohitajika kabla ya kufikia mwezi Februari, 2023.
Kufuatia amri hiyo, Puttin pia ameiagiza Serikali kutenga pesa za kugharamia wigo mpana wa kikosi hicho, huku baadhi ya wachambuzi wakielezea hatua hiyo kuwa ni ishara tosha kwamba, “baada ya miezi sita kamili ya mapigano, Putin hakuwa na mpango wa kulega.”
Inadaiwa kuwa, Putin pia anaweza kujaribu kuvijenga upya vikosi vyake na tayari Wataalamu wamehusisha kasi ya kupungua kwa mashambulizi ya Urusi na ukosefu wa wafanyakazi huku makadirio ya Magharibi ya wahasiriwa wa Urusi, pamoja na vifo na majeruhi, yakifikia watu 80,000.
Amri hiyo ya Putin, inawakilisha mabadiliko ya kushangaza juu ya juhudi za miaka kadhaa za Kremlin kupunguza jeshi lenye idadi kubwa ya watu, ingawa rasimu ya kitaifa ingeharibu hali ya kawaida ambayo Urusi imetaka kudumisha, licha ya vikwazo vya kiuchumi na kuendelea kwa mapigano.