Zaidi ya watu 340,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Chad tangu mwishoni mwa mwezi Juni, kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), imesema, “Aida ya muda kutokana na mafuriko ni watu 341,056 walioathirika (kaya 55,123), katika majimbo 11 kati ya 23, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa N’Djamena.

Mvua kubwa imekuwa ikiathiri nchi hiyo ya Afrika ya kati kwa wiki kadhaa ambapo watu walioathirika zaidi ni wale ambao wamelazimika kutelekeza nyumba zao na kupoteza mali huku watu kadhaa wakipata majeraha, maradhi na kupoteza maisha.

Raia wa Chad katika moja ya mitaa iliyokumbwa na Mafuriko. Picha na Aurelie Bazzara -Kibangula/AFP.

Ocha imefafanua kuwa, katika kumbukumbu zilizohifadhiwa, zinaonesha kuwepo kwa visa zaidi miaka ya nyumba na kusema, “ikumbukwe kwamba watu 256,000 waliathiriwa na mafuriko mwaka 2021 na 388,000 kwa mwaka 2020.”

Mapema Agosti 19, 2022 Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, ilitangaza kuwa watu 22 wamefariki tangu kuanza kwa mwezi Juni nchini Chad kwa sababu ya mvua kubwa.

Msaada unaohitajika unakaribia kufikia dola milioni 6.3, ambapo Serikali ya nchi hiyo ina kiasi cha dola milioni 1.1 pekee, huku Ocha ikisema haiwezi kukabiliana na hali hiyo, na kwamba inahitaji misaada zaidi kitu kilichowafanya kutoa wito kwa wafadhili.

Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, imesema hadi kufikia mwaka 2021, Wachadi milioni 5.5, au zaidi ya theluthi moja wangehitaji msaada wa dharura wa kibinadamu kutokana na kadhia iliyowapata.

Wanahabari kuwa jicho la matumizi ya dawa
Mdee na wenzake 18 watinga Mahakamani