Rapa mahiri nchini Nigeria, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Penthauze Music, Chibuzor Nelson maarufu Phyno ameiachia rasmi rekodi yake mpya ‘Full Current’ (That’s My Baby) ambayo amemshirikisha mwanamuziki na mtayarishaji mahiri kutoka nchini Nigeria Tekno Miles.
‘Full Current’, ni moja ya rekodi za Phyno ambaye pia ni mshindi wa tuzo mbali mbali za muziki barani Afrika iliyo na mahadhi ya Amapiano yenye ikitaja sifa za mwanamke mrembo.
Kwa mara ya kwanza rapa huyo kutoka nchini na Nigeria anaibua gumzo kwa mashabiki na wadau wa muziki hasa baada ya kutangaza kuwa rekodi hiyo inajumuisha mirindimo ya muziki kutoka Afrika ya kusini.
Huku idadi kubwa ya mashabiki wakionyesha kushtushwa na aina hiyo ya muziki huo kufanywa na Phyno zaidi ni kutokana na mirindimo ya wimbo huo, kuwa nje ya fikra za wengi wenye kufuatilia muziki wa rapa huyo.
Hata hivyo, mashabiki wengi wameonekana kuibua mijadala kupita kwenye majukwaa mbali mbali ya kusikiliza muziki Online ambako rekodi hiyo imewekwa.
Mwaka 2021, rapa huyo kutoka Nigeria aliachia albamu yake ya nne iitwayo SOMETHING TO LIVE FOR, ambayo ilikuwa miongoni mwa albums zilizomuweka kweye nafasi kubwa kimuziki, barani Afrika.
Ikumbukwekuwa, rapa Phyno amewahi kushiriki kwenye wimbo uitwao ‘Body’, moja ya rekodi inayopatikana kwenye album ya kwanza na msanii Harmonize ‘Afro east’iliyotoka mapema mwaka 2020.