Katika tukio la kushtua, Mwanahabari Mtangazaji Kate McKean wa uingereza alianguka na kuzirai wakati wa mdahalo wa wagombea wa nafasi ya Waziri Mkuu nchini humo uliokuwa ukipeperushwa moja kwa moja Jumatano, Julai 27, 2022.

Mdahalo huo ambao ulikuwa kati ya wagombea wa nafasi ya uwaziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Liz Truss na kusababisha mdhahalo huo kukatishwa.

Mwanahabari Mtangazaji Kate McKean(katikati) wakati wa mdhahalo wa wagombea wa Waziri Mkuu Uingereza. Picha: Euronews.

Wakati wa tukio hilo, Liz Truss alikuwa akijibu swali kuhusu vita vya Urusi na Ukraine na Rais Putin kisha kulisikika sauti kubwa ya mlipuko au mdondoko na ya kushtua.

Truss alionekana kwenye televisheni akiwa amepigwa na mshangao wa ghafla na kuweka mikono yote juu ya uso wake na kusema “Oh Mungu wangu!” Ingawa Sekunde chache baadaye, alitulia, kukawa kimya akaenda hadi upande ambao mtangazaji alipokuwa.

Mdhahalo huo ambao ulikuwa uendelee kwa saa moja, ulikatishwa na kisha kipindi kikafungwa na baadae katika Taarifa za Televisheni hiyo taarifa ilisema kwamba Msimamizi Kate McCann alizimia hewani na ingawa yuko sawa, ila ushauri wa matibabu ulisema mjadala usiendelee.

Tukio hilo linatokea huku mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa Chama cha Conservative ukiendelea, ambaye pia atakuwa Waziri Mkuu ajaye wa Uingereza.

Waziri wa Fedha wa Uingereza na mwenye asili ya India Rishi Sunak na waziri wa mambo ya kigeni Liz Truss wanapigania kumrithi Boris Johnson ambaye alijiuzulu kama kiongozi wa Chama tawala cha Conservative mnamo Julai 7, baada ya miezi kadhaa ya kashfa za maadili na kusababisha kuhama kwa mawaziri kutoka kwa serikali yake.

Msukosuko huo ulianza baada ya kuzuka kwa kashfa ya unyanyasaji wa kingono inayomuhusisha mbunge wa Conservative Chris Pincher ambaye ni mshirika wa karibu wa Johnson.

Mayele: Nipo Young Africans kihalali
Uhuru agoma kumkabidhi Ruto nchi