Wakati ulimwengu wa sanaa ya muziki ukiendelea na mjadala mzito kuhusu madai ya kupoteakama si kufa kabisa kwa muziki wa R&B duniani, mjadala ulioanzishwa na nyota wa muziki wa Hip hop kutoka nchini Marekani P Diddy.
Kwa upande wa pili, kumeibuka mjadala mwingine uliozalisha taswira sawa na hiyo wenye kushindanisha ni yupi msanii bora na mahiri wa muziki wa R&B wa muda wote kati ya mwimbaji Usher Raymond pamoja na R-Kelly ambaye kwasasa yuko gerezani akitumikia kifungo kufuatia kesi kadhaa ikiwa ya unyanyasaji wa kingono zinayomkabili.
Mjadala huo mpya, umekuja kufuatia kauli ya mwanamuziki YKOsiris ambaye kupitia kwenye mahojiano yake na DjVlad, ametolea majibu kauli ya ya rapa Boosie iliyodai kwamba “hakuna binadamu yeyote kwa sasa anayeweza kumshinda R-Kelly kwenye jukwaa la Verzuz.
“R-Kelly ni mmoja wa wasanii wakali na wakubwa, lakini kwa upande wangu namkubali Usher Raymond. Ni kweli kuwa R-Kelly ni moto lakini kuna baadhi ya vitu kwake vinanikata, Najikuta namkubali Usher tu, R-Kelly amefanya mengi yasiyokuwa na maana” – amesema YKOsiris
Punde baada ya kuenea kwa sehemu ya mahojiano hayo, mashabiki na wadau mbali mbali wa muziki duniani walebeba suala hilo na kila mtu kuweka waz mtazamo wake kuhusu uhodari walionao wasanii hao na ni yupi hasa mwenye kufaa kutwika taji la ufalme wa muziki wa R&B.