Kampuni ya Capitol Records, imeingia kwenye headlines za Duniani baada ya kuripoti habari za kuwa record label ya kwanza kumsaini mwanamuziki ambaye ni Roboti (The artificial intelligence rapper) aitwaye FN Meka.

Msanii huyo mpya, aliachia wimbo wake wa kwanza na Gunna pamoja na mtangazaji Clix inayoitwa ‘Florida Water’. Rapa huyo ametengenezwa na kampuni ya rekodi ya mtandaoni ya Factory New.

Mwanzilishi mwenza wa kampuni hiyo, Anthony Martin, alielezea mchakato wa kutengenezwa kuwa roboti hilo jinsi ulivyokuwa, huku akiiweka wazi dhamira yao alipokuwa katika mahojiano mapema mwaka jana 2021 ambapo alisema kuwa.

“Mfano wa zamani wa kutafuta talanta haufai na hautegemewi tena kwa sasa, ilikuwa inahitaji kutumia muda kuvinjari mtandaoni, kusafiri kwenye maonyesho, kuruka na ndege hadi mikutanoni, kutumia rasilimali zote kutafuta mchanganyiko wa mahiri wa sifa ambazo anazostahili msanii mpaka kufikia hatua ya kuitwa nyota.

Lebo zote za pesa zinazojitolea kutafuta talanta, kiwango cha mafanikio ni 1% ambayo ni ya kusikitisha, sasa tunaweza kuunda wasanii maalum kwa kutumia vipengele vilivyothibitishwa kufanya kazi, na kuongeza uwezekano mkubwa wa mafanikio.

Hata kama tunaweza kufikia kiwango cha mafanikio cha 2% basi tutakuwa tumeongeza kiwango cha tasnia mara mbili. aliesema Anthon.

Ameendelea kudokeza kuwa angependa kuona wanafanya maboresho zaidi kwa roboti hilo ili kufikia hatua ya kubadilika kwenye kuimba kwa sauti ya binadam hadi kuanza kuzalisha sauti yake binafsi itokanaoyo na kompyuta ili roboti hilo liwe limekamilika sawa na msanii mwingine yeyote.

“Kufikia sasa, sauti ya mwanadamu ndiyo inayoimba, lakini tunafanya kazi kuelekea kuwa na uwezo wa kzalisha sauti yake maalumu kupitia kompyuta ili roboti hili lianze kuja nakuja maneno yake binafsi, na hata kushirikiana na kompyuta nyingine kama “waandishi-wenza.” Aliongeza Anthon.

Roboti hilo kwa sasa linaendelea kujizolea umaarufu mkubwa duniani huku nje ya matarajio ya wengi, limefanikiwa kupata zaidi ya wafuasi 10 milioni kwenye mtandao wa TikTok muda mfupi tangu kutambulishwa kwake rasmi.

R-Kelly na Usher Raymond wazua gumzo jipya
Sensa: Utulivu watawala zoezi likiendelea