Waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni amesema kuwa mmoja wa wanawake waliouawa kwa bunduki mwishoni mwa juma jijini Roma alikuwa rafiki yake.

Mwanamke huyo ambaye Waziri Mkuu Meloni amemtaja kwa jina moja la Nicoletta, pamoja na wenzake wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na mwanamme mmoja, kwenye baa iliyo upande wa kaskazini wa mji wa Roma Desemba 11, 2022.

Katika tukio hilo, watu wengine wanne wamejeruhiwa katika shambulizi hilo lililoishtua Italia ambapo pia muuaji huyo aliwashambulia majirani zake waliokuwa wamekusanyika, na inaarifiwa kuwa alikuwa tayari amewatishia watu wanaoishi kwenye jengo moja.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 57, alikuwa amechapisha kwenye blogu yake kwamba anawachukia majirani na tayari amekamatwa, huku Waziri Mkuu amesema sheria itachukua mkondo wake.

Makamu wa Rais kizuizini kwa makosa ya ufisadi
Shambulizi Hotelini lachukua uhai wa watatu