Raia wa Libya, Abu Agola Mohammad Masud anayetuhumiwa kwa kutengeneza bomu lililoilipua ndege ya Pan Am kwenye anga ya Scotland mwaka wa 1988, amewekwa kizuizini nchinib Marekani.

Kwa mujibu wa waendesha mashitaka wa Marekani na Scotland, Abu alishitakiwa na Marekani, kwa ulipuaji wa ndege hiyo kwenye mji wa Lockerbie ambapo hapo awali, Abu alikuwa anazuiliwa Libya, kwa madai ya kuhusika na shambulizi la mwaka wa 1986 katika klabu moja ya usiku mjini Berlin.

Picha ya mmoja wa wahusika na tukio analodaiwa kuhusika nalo. Picha ya Daily record.

Msemaji wa Ofisi ya Mwendesha mashitaka wa Scotlnad amesema familia za waliouawa katika mlipuko wa Lockerbie wamefahamishwa kuwa mshukiwa Abu Agila Mohammad Mausud Kheir Al-Marimi yuko kizuizini Marekani.

Amesema Maafisa wa Scotland, Uingereza na Marekani kwa pamoja wanaendelea na uchunguzi ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria walioshirikiana na Al-Megrahi ambapo Ndege hiyo ya Pan Am nambari 103 ililipuka Desemba 21,1988 na kuwauwa watu 270.

Diamond, The Game mbioni kuachia 'goma jipya'
Miili ya watu 27 yatupwa barabarani