Kitendo cha Raila Odinga kujiapisha kimeibua maswali mengi likiwemo kitu gani kitafuata baada ya kuonekana kufanya kosa kisheria.
Japo wapo wanaosema kuwa Odinga hajafanya kosa kisheria la uhaini kwani hajajiapisha kama Rais wa Kenya isipokuwa ni Rais wa watu wa Jamhuri ya Kenya.
Maneno yaliyotamkwa kwenye kiapo hicho yanasema kwamba …”Mimi, Raila Amolo Odinga, kwa kutambua wito wa juu kuchukua madaraka ya Rais wa Watu wa Jamhuri ya Kenya, naapa kuwa nitakuwa mwaminifu na kuwa na utii wa kweli kwa watu na Jamhuri ya Kenya, kwamba nitahifadhi, kulinda na kulinda Katiba ya Kenya, kama ilivyowekwa na sheria na sheria nyingine zote za Jamhuri kama ilivyopitishwa na Watu wa Kenya; Nitawalinda na kuendeleza uhuru na heshima ya Watu wa Kenya. Basi nisaidie Mungu”, yalisikika maneno haya yakitamkwa kinywani mwa Odinga.
Tukio hilo lilihudhuriwa na maelfu ya Wakenya kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo, huku baadhi ya viongozi wengine wa Nasa ambao nao walitakiwa kuwa miongoni mwa wanaoapa kuikacha na kuingia mitini, akiwemo Kalonzo Musyoka na Mudavadi.
Baada ya hapo Raila Odinga alibadilisha status yake ya twitter na kuweka kama Rais wa Kenya, lakini baadaye alibailisha na kuweka kama Rais wa watu.
Kwa mujibu wa sheria za Kenya, mtu ambaye ataapa kuwa Rais wakati bado kuna Rias mwengine madarakani aliyewekwa kisheria na katiba ya nchi hiyo, anafanya kosa la uhaini ambalo hukumu yake ni kunyongwa.
Mpaka sasa serikali ya Kenya haijatoa tamko lolote juu ya kitendo hicho cha Raila Odinga, ambacho watu wengi wana shauku ya kutaka kujua nini kitafuata? Je, atashtakiwa au ataachwa huru!?