Mshambulia wa Kimataifa kutoka Tanzania, Mbwana Samatta amerejea uwanjani kuitumikia timu yake ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubeligiji kwa kutoa pasi ya bao la kwanza wakati timu yake ikifungwa ugenini 3-2 na Kortrijk Kwemye mchezo wa Kombe la Ubeligiji Guldensporen

Samatta ambaye alicheza kwa dakika 75 kwenye mchezo huo, alikuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili kufuatia kupata maumivu ya mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia aliyoyapata mwezi Novemba mwaka jana.

Hata hivyo, huo ni mchezo wa pili kwa mshambuliaji huyo kucheza tangu atoke majeruhi, mechi ya kwanza ni ile ya Ligi, ambayo aliingia dakika saba za mwisho kuchukua nafasi ya Mkosovo Edon Zhegrova, huku timu yake ya Genk ikilazimishwa sare ya 1-1 na Sint-Truiden Januari 27.

Wema kuja kivingine Juni 30, 2018, Diamond amsapoti
Raila aapishwa kama Rais wa watu, wengi wahoji