Aliyekuwa Rais wa Yemen, Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na washirika wake wa zamani.
Shirika la habari linalomilikiwa na waasi wa Houthi limesema kuwa mwisho wa matatizo na mizozo katika eneo hilo ni kiongozi wao.
Wiki iliyopita, wafuasi wa Saleh walikuwa wanapigana pamoja na wapiganaji wa jamii ya Houthi dhidi ya rais wa sasa wa Yemen Abdrabbuh Mansour Hadi.
Aidha, uhasama wa muda mrefu wa kisiasa pamoja na mzozo kuhusu udhibiti wa msikiti mkuu katika mji mkuu wa Sanaa unaodhibitiwa na waasi vilichangia mapigano makali ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 125 na wengine 238 kujeruhiwa vibaya.
Hata hivyo, Watu zaidi ya 8,670 wameuawa na wengine 49,960 kujeruhiwa tangu majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yalipoingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe Machi 2015, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.