Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir ameagiza kuachiwa kwa wafungwa wote wa kisiasa wanaoshikiliwa kwenye magereza nchini humo.
Uamuzi huo umekuja wakati ambapo vyama vya siasa na makundi ya asasi za kiraia nchini humo vimeshiriki mijadala ya kitaifa inayoendelea ikihusisha wawakilishi wa Serikali.
Bashir ambaye ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 1989 amesema kuwa hatagombea tena urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
“Kuwaachia wafungwa wote wakisiasa ni juhudi za kuimarisha umoja wa kitaifa na amani inayohuishwa na mjadala wa kitaifa unaoendelea kama sehemu ya maandalizi ya katiba ya nchi,” shirika la habari la SUNA limeripoti.
Mbeya City kuwavaa Simba bila Hassan Mwasapili, John Kabanda
Wanasiasa, viongozi wa dini watajwa kwa Makonda kutelekeza watoto
Tangu mwaka 2015, Serikali ya Bashir imekuwa ikifanya mikutano na viongozi wa upinzani pamoja na makundi ya waasi kupitia mijadala ya kitaifa. Hiyo ni sehemu ya juhudi za kumaliza migogoro inayoendelea katika maeneo yenye vita kama Darfur.