Mabeki muhimu wa klabu ya Mbeya City Hassan Mwasapili na John Kabanda  wameshindwa kusafiri na kikosi kuelekea Dar es salaam, kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba SC utakaochezwa kesho Alhamisi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Mbeya City Ramadhani Nswanzurimo amesema, amelazimika kuwaacha wachezaji hao kwa sababu tofauti, ambapo kwa upande wa nahodha Hassan Mwasapili anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano ili hali John Kabanda ni majeruhi.

Hata hivyo kocha huyo kutoka nchini Burundi, amesema suala la kukosekana kwa wachezaji hao wawili, hakutoharibu mipango yake ya kuhakikisha anashinda ugenini dhidi ya Simba na kujiongezea alama kwenye msimamo wa ligi kuu.

Amesema nafasi za Mwasapili na Kabanda zitajazwa na mabeki wengine, Haruna Shamte na Rajab Isihaka.

“Nitawakosa wachezaji hao wawili, kwa kuwa nina wachezaji wengi ninaimani watachukuwa nafasi zao na kutendea haki,” alisema.

Mbeya City watashika dimbani hiyo kesho huku wakiwa na kumbukumbu ya kuambulia matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Azam FC, mwishoni mwa juma lililopita mjini Mbeya, jambo ambalo kocha Nsanzurumo amesema limeongeza chachu ya kupambana kikosini kwake.

“Tunahitaji kupata alama katika kila mchezo ili tujiweke katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi, tukilenga alama nyingine dhidi ya Simba katika mchezo wa kesho,” alisema Nswanzurimo.

Kwa upande wa Simba watakua wanachagizwa na ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya jumatatu, huku dhumuni lao kubwa litakua ni kuendeleza moto wa ushindi mbele ya Mbeya City, ili kufikia lengo la kutwaa ubingwa msimu huu wa 2017/18.

Rais awaachia huru wafungwa wote wa kisiasa
Video: Wananchi watakiwa kupima afya zao