Rais wa Marekani, Biden ameahirisha ziara yake ya Jordan akiwa njiani kuelekea Israel, baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye Hospitali moja mji wa Gaza na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Biden alikuwa njiani kuelekea Mashariki ya Kati, kujaribu kutafuta suluhisho la kusitisha ghasia zinazoendelea kati ya Israel na Hamas, ndipo serikali ya Jordan ilipotangaza kwamba mkutano wa kilele ulopangwa kufanyika hii leo Oktoba 18, 2023 kati yake na Viongozi wenzake wa Jordan, Misri na Palestina umeahirishwa.

Aidha, uamuzi huo ulichukuliwa baada ya Rais wa Palestina, Mahamoud Abass kuamua kuondoka Amann ambako alipanga kuhudhuria mkutano huo akiwa amekasirishwa na shambulio dhidi ya Hospitali inayosimamiwa na Kanisa la Batist mjini Gaza, la Al-Ahli Arab.

Hata hivyo, kila upande katika vita hivyo vya Ukingo wa Gaza umekana kuhusika na shambulio hilo na wanaendelea kushutumiana kwa mlipuko huo mkubwa ambapo Maafisa wa Palestina wanasema zaidi ya watu 200 waliuliwa kutokana na shambulio hilo.

FAO yaunga mkono juhudi uendelezaji sekta ya Kilimo
Tanzania ina fursa ya Kilimo, uchumi wa Buluu - Dkt. Qu