Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo – FAO, limeahidi kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 hadi  Oktoba 20, 2023 wakiti akihutubia mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zina mipango ya kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula ndani ya nchi na ziada kuuza nje ifikapo 2030.

Kabla ya ufunguzi wa mkutano huo uliowahusisha Wakuu wa nchi na Serikali, Waziri Mkuu alishiriki katika Maadhimisho ya miaka 78 tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo la FAO na kudai kuwa Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara na nishati vijijini, ili kurahisisha shughuli za kilimo.

Serikali kuwainua Wawekezaji wa ndani - Mahawanga
Rais Biden chupuchupu Jordan