Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari ameunga mkono mpango wa kuwafukuza kazi zaidi ya walimu 20,000 ambao walifeli mitihani katika jimbo la kaskazini la Kaduna nchini humo ili liwe fundisho kwa wengine.
Gavana wa jimbo hilo wiki iliyopita alichapisha makaratasi yaliyokuwa yamesahihishwa kwenye mtandao wa Twitter akisema kuwa walimu hao walikuwa wamefeli mtihani wa darasa la nne ambao unastahili kufanywa na wanafuzi wa umri wa miaka 10.
“Ni jambo la kusikitisha kuwa mwaimu hawezi kufaulu mitihani ambayo inastahili kufanywa na watoto, jambo ambalo ni aibu kubwa katika taifa lililoendelea kama hili, hivyo naunga mkono hatua iliyochukuliwa dhidi yao,”amesema Buhari.
Amesema kuwa walimu hao wamefukuzwa kazi lakini wanaweza tena kutuma maombi upya katika shughuli fani zingine ili waweze kufanya kazi zingine za ujuzi wao unaostahili lakini sio ualimu.
-
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe akimbia, Mke wa Mugabe atajwa kumrithi
-
Wanne wakamatwa kwa kumzomea mke wa Rais
-
Jeshi ‘labisha hodi’ mgogoro wa madaraka Zimbabwe
Hata hivyo, ameongeza kuwa maombi ya kazi 19,000 yamepokelewa ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya walimu hao kufukuzwa kazi kwa kufeli mtihani huo.