Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema wameazimia kuweka mazingira yatakayofanya biashara kati ya Tanzania na Zambia zisiwe na vikwazo.

Wakizungumza katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia, wamesema eneo moja la muhimu ni kuhakikisha magari hayakai kwenye mipaka kwa muda mrefu pasi na sababu.

Marais hao, wamekutana kwenye mkutano wa ana kwa ana leo asubuhi na waliwaambia Wafanyabiashara hao kwamba, mazungumzo yao yatajikita kwenye kuweka taratibu za kuondoa changamoto hizo.

Jana, Oktoba 24, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema Tanzania itatenga eneo la ekari 20 katika mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhudumia mizigo kutoka Nchini Zambia.

Chelsea, Man City zapigana vikumbo
Kisasi: Waasi watumia mapanga kuuwa 26 DRC