Rais wa Zambia, Edga Lungu ametoa amri ya kila mwananchi wa nchi hiyo ni lazima afanyiwe vipimo vya ugonjwa ukimwi ili kuweza kujua ni jinsi gani anaweza kusaidiwa asiweze kusambaza maambukizi kwa wengine.
Rais huyo amefikia hatua hiyo mara baada ya nchi hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo kusini mwa bara la Afrika ikiwa na asilimia 11.6 huku watu walio na umri wa miaka kuanzia 15 mpaka 49 wakiishi na virusi vya ukimwi.
Aidha, Lungu ameongeza kuwa kupimwa ukimwi na kupewa ushauri pamoja na matibabu si jambo hiari bali ni lazima kwakuwa zoezi hilo limelenga kuweza kupunguza maambukizo ya ugonjwa huo nchimi humo.
-
Zuma: misimamo yangu ilitaka kunisababishia kifo
-
Korea Kaskazini yatoa ripoti ya uamuzi kuishambulia ardhi ya Marekani
-
Odinga ashindwa kutangaza msimamo wa NASA
Hata hivyo, Lungu ametangaza agizo hilo katika uzinduzi wa baraza la ukimwi lililofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Lusaka ambapo amesema suala hilo pia lilijadiliwa na baraza la mawaziri.