Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa jimboni kwake wa jamii ya kifugaji kuacha tamaduni zao za kutowapeleka watoto shule na kuwatumikisha kufuga mifugo yao.
 
Nchemba amezitaka jamii hizo kuachana na tamaduni ambazo zimepitwa na wakati kwani hali ya maisha imebadilika tofauti na miaka iliyopita ambapo kulikuwa na sehemu kubwa ya kufugia mifugo yao lakini sasa mabadiliko ya tabianchi yanasababisha ukame hivyo amewaasa kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto shule ili waje kuwa msaada kwa baadaye.
 
Aidha, katika kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto shule amejitolea kusomesha watoto katika ambao wameshindwa kuendelea na shule kwasababu ya wazazi wao kufariki, na wengine kuwa hali ya ulemavu.
 
  • Eng. Ngonyani acharuka, aipa miezi mitatu TPA
  • Prof. Ole Gabriel: Vyombo vya habari shirikianeni na BAKITA
 
Hata hivyo, katika ziara yake hiyo ya jimboni kwake, Nchemba ametembelea ujenzi wa hosteli katika kila shule ya Sekondari katika Kata 20 na kujionea maendeleo ya ujenzi huo ambao unaendelea kwa kasi kubwa

Rais Edga Lungu: Kupima ukimwi si jambo la hiari
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 16, 2017