Rais wa Marekani Joe Biden ametetea uamuzi wake wakuondoa majeshi ya ya nchi hiyo kutoka Afghanistan baada ya wanamgambo wa Taliban kuchukua udhibiti wa Serikali.
Ametetea uamuzi huo alipokuwa akihutubia Taifa hilo kwa njia ya televisheni eneo la ikulu ya Marekani (White House), Biden amesema oparesheni ya Marekani nchini Afghanistan kamwe haikuwa kujenga Taifa na kusema tishio la ugaidi ambalo lililipeleka jeshi la Marekani katika nchi hiyo limevuka nje ya Afghanistan.
Biden amekuwa akitetea uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini humo ifikapo Agosti 31., amekiri kwamba ushindi wa Taliban kote nchini Afghanistan umetokea, “kwa haraka sana kuliko ilivyotarajiwa.”
Hata hivyo, Biden amesema, ni kosa kuamuru wanajeshi wa Marekani kujihusisha katika mapambano zaidi, wakati wanajeshi wa Afghanistan hawako tayari kufanya hivyo.