Rais wa Rwanda, Paul Kagame anatarajia kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika mkutano mkuu wa masuala ya kiuchumi, World Economic Forum WEF unaofanyika Davos Uswizi.
Kagame atakuwa kiongozi pekee kutoka Bara la Afrika atakayekutana na Trump kulingana na ratiba iliyotolewa na mshauri wa masuala ya kiusalama wa Marekani H.R McMaster.
Aidha, Wawili hao wanatarajia kukutana siku ya Ijumaa huku kukiwa na malalamiko makubwa dhidi ya Trump ambaye aliyataja mataifa ya Afrika kuwa ni ‘machafu’ au ya ‘Mabwege’ katika mkutano wa kuzungumzia sera ya uhamiaji.
Mkutano wa rais Trump na Kagame, ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika utaimarisha uhusiano wa Afrika na Marekani, ambapo wanatarajia kuzungumzia masuala muhimu ikiwemo biashara na usalama.
Hata hivyo, Trump pia anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May na rais wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Davos.