Daktari wa timu ya Olimpik, Larry Nasser amehukumiwa kifungo cha jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi ya wananawake na wana michezo.

Katika kesi hiyo mashahidi 160 wamewasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe amekiri makosa kumi.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo, Larry alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha za ngono za watoto kinyume cha sheria.

Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine.

‘Nataka ukae jela maisha yako yote’. Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mmoja wa waathirika amesisitiza kuwa washirika wa daktari huyo wanapaswa kushitakiwa pia.

Hukumu ya Larry Naser inafuatia wiki ya ushuhuda kutoka kwa wanawake takribani mia moja na sitini, wakiwemo washindi wa medali ya dhahabu ya olympiki Biles, Aly Raisman, Gabby Douglas na McKayla Maroney

Video: Tundu Lissu nimetolewa risasi nyingine mwilini, Wabunge 11 wasota kizimbani
Rais Kagame kuteta na Trump kuhusu Afrika