Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro anakabiliwa na tuhuma za kujihusisha na upokeaji rushwa kutoka katika kampuni moja ya ujenzi nchini humo.
Hayo yamesemwa na Muendesha mashitaka wa zamani wa nchi hiyo, Luisa Ortega Diaz alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ushahidi anao kwamba Rais Nicolous Maduro na kundi la maofisa wengine walipokea hongo kutoka kampuni hiyo ya ujenzi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Brasilia, Ortega amewataja wanaotuhumiwa kuchukua hongo kuwa ni pamoja na Rais Maduro, Makamu Rais chama tawala Diosdado Cabello na kiongozi mwingine wa chama Jorge Rodriguez.
Aidha, hatua hiyo imefikiwa mara baada ya makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence kusema kuwa utawala wa Rais Trump unatarajia kuongeza nguvu dhidi ya Venenzuela ili kurejesha utawala wa kidemokrasia.
-
Marekani, Korea Kusini zaungana kufanya mazoezi ya kijeshi
-
India yafuta sheria ya kuwapa talaka wanawake kirahisi kwa ‘WhatsApp’
-
Elimu bure ya JPM yaikuna Uingereza
Hata hivyo, makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amesema kuwa kama Venezuela itaingia kwenye mgogoro unaofukuta kwa sasa basi kutaathiri ukanda mzima na kusababisha ongezeko la usafirishaji wa dawa za kulevya na ongezeko la wahamiaji haramu.