Rais John Magufuli jana alimtuma rasmi mteule wake, Mrisho Gambo kuwa muwakilishi wake katika mkoa wa Arusha ambao unatajwa kuwa na changamoto nyingi kiutendaji.

Rais alimuapisha rasmi Gambo Ikulu jijini Dar es Salaam, katika tukio lililohudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo.

Rais Magufuli na Gambo, Ikulu

Gambo amekabidhiwa mkoa wa Arusha baada ya kuonekana kufanya vizuri katika nafasi yake ya Ukuu wa Wilaya ya Arusha, licha ya kukutana na changamoto kubwa ya kuvutana na Baraza la Madiwani linaloongozwa na Chadema.

Mkuu huyo mpya wa Mkoa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Felix Ntibenda ambaye amerudishwa Ofisi ya Waziri Mkuu akisubiri kupangiwa kazi nyingine.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema juzi alikosoa uteuzi huo akimshambulia Gambo kuwa hajui kufuata taratibu na kwamba anavunja amani ya Jiji hilo.

Akiwa bado ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gambo alisikika akiwatahadharisha Chadema kutothubutu kufanya maandamano na Mikutano, Septemba Mosi akidai kuwa yeye ndiye ‘kiboko’ wa oparesheni yao ya ‘Ukuta’.

CCM wataka Maalim Seif azuiwe kuhudhuria matukio ya kitaifa
Lowassa atoa neno kwa Serikali kuhusu shule zinazoungua moto