Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa aliyekuwa anagombania nafasi hiyo kwa kipindi cha awamu ya pili, ameshinda kwa asilimia 52.6 dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa aliyepata asilimia 44.
Matokeo hayo ya Uchaguzi mkuu nchini humo yametangazwa usiku wa kuamkia leo Jumapili Agosti 27, 2023.
Mnangwagwa alikuwa akipeperusha bendera ya chama cha ZANU-PF, huku mpinzani wake wa karibu Chamisa akipeperusha bendera ya CCC.
Japokuwa matokeo hayo yametangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo, bado upande wa upinzani na baadhi ya waangalizi wa nje wameonyesha kutokuridhika nayo.