Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Ikulu ya Entebbe nchini humo, ili kupokea salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Nchi ya Uganda.

Mara baada ya kupokea salamu hizo, Rais Museveni ameishukuru Serikali ya Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa na mafanikio makubwa ya kihistoria na kiuchumi.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Doto Biteko ukiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Rais Yoweri Museveni (hayupo pichani) Ikulu ya Entebbe nchini Uganda.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu Biteko alikabidhi zawadi kwa Rais Museveni, kama njia ya kuthamini mchango na ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda.

Rais Yoweri Museveni akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko Ikulu ya Entebbe nchini Uganda.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe Balozi Stephen Mbundi pamoja na viongozi wengine kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.

Umeme Vijijini kuboresha viwango vya Elimu - Kapinga
Chongolo kuibana Serikali ujenzi Lyamba lya Mfipa