Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kesho, Julai 13 anatarajia kufanya ziara binafsi nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo, Rais Museveni atamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Kijijini kwake Mlimani, wilayani Chato, mkoani Geita.

Akiwa kijijini hapo, Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli. Ikumbukwe hivi karibuni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alimtembelea Rais Magufuli nyumbani kwake, ambapo alifanya mazungumzo naye binafsi.

 

Video: Fahamu njia rahisi ya kuwa salama mahali pa kazi
Video: Aliyekataliwa na baba aongoza kidato cha 6, Wasichana wang'ara kidato cha 6 nchini