Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameondoa vikwazo vyote vya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola, amesema kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki imepiga hatua katika kukabiliana na ugonjwa huo hatari.
Pia Museveni, amefuta vikwazo vya kitovu cha ugonjwa huo katika wilaya ya Mubende, ambayo ilikuwa na jumla ya visa 66 na vifo 29, na katika mkoa wa Kassanda wenye visa 49 na vifo 21.
“Kwa sasa, hakuna maambukizi, hakuna wathiriwa wanaofuatiliwa, hakuna wagonjwa katika vituo vya kutengwa, na tunaendelea vyema na hesabu kupungua,” amesema Museveni
Maafisa wa afya walithibitisha kwa mara ya kwanza mlipuko wa ugonjwa huo mnamo Septemba 2022, na kusema kuwa ni aina ya ugonjwa wa Sudan, ambao unaua kwa 40% -60% ya wale wanaoambukizwa, na ambao hauna chanjo iliyothibitishwa.
Mnamo Oktoba, serikali ya Uganda iliweka vikwazo vya usafiri na amri ya kutotoka nje usiku mmoja na pia kufunga maeneo ya ibada na burudani.
Mapema Disemba 2022, Uganda ilisema imemruhusu mgonjwa wake wa mwisho wa Ebola kuondoka hospitalini.
Kifo cha kwanza kurekodiwa kutokana na ugonjwa huo kilikuwa cha mwanaume mwenye umri wa miaka 24, kutoka Mubende ambapo pia ndugu zake sita pia walifariki.
Kifo kingine pia kilirekodiwa mwezi huu katika mji mkuu wa Kampala ambaye anadaiwa alisafiri akitokea Mubende, hata hivyo, wilaya tano ndizo zilizo na maambukizi.