Rais Mwinyi amteua Makamu wake kuwa Mwenyekiti Tume ya udhibiti Dawa za Kulevya
4 years ago
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Abdulla kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya.
Uteuzi wa Abdulla ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar umeanza leo Juni 24, 2021.