Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema usafiri wa baharini ni muhimu katika nchi kama Zanzibar, na Serikali inafanya juhudi za kuimarisha miundombinu na mazingira ya huduma za usafiri wa baharini.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati wa uzunduzi wa boti mpya Kilimanjaro VIII hii leo Aprili 24, 2023 na kuongeza kuwa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma una umuhimu katika kukuza uchumi na kuimarisha huduma za jamii ikiwa ndio malengo ya Serikali.

Amesema, malengo ya Serikali ni kuzipatia ufumbuzi wa muda mrefu changamoto zitokanazo na msongamano wa abiria , ufinyu wa nafasi wa bandari kuu ya Malindi kwa kutekeleza mradi wa ujenzi kisasa wa Ferry Terminal eneo la Maruhubi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.

Aidha, Rais Mwinyi pia ameiomba kampuni ya Azam Marine kufanya safari kati ya Unguja na Pemba ikiwezekana na Mkoa wa Tanga Tanzania bara ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri.

Magonjwa yasiyoambukiza kuandaliwa mtaala - Dkt. Mollel
Tanzania kushirikiana na Korea utengenezaji Filamu bora