Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, David Concar kwa mazungumzo.
Rais Mwinyi amekutana na Kiongozi huyo hii leo Mach 30, 2023 Ikulu, mjini Zanzibar ambapo katika mazungumzo hayo waligusia ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Pemba.
Balozi huyo wa Uingereza, alimwambia Rais Dkt. Mwinyi kuwa mchakato wa fedha wa mradi wa ujenzi huo wa Kiwanja cha Ndege unakwenda vizuri.
Nchi ya Uingereza ni mshirika mkubwa katika ujenzi wa mradi huo utakaotekelezwa huko Pemba.