Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameutaja ugonjwa wa Uviko-19 kuwa moja ya mambo magumu aliyopambana nayo alipoingia madarakani.

Ameyasema hayo leo Novemba 6, 2021 katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani Novemba 2020.

Dkt. Mwinyi ameutaja ugonjwa wa Uviko-19 kusababisha mdororo mkubwa wa uchumi hususani nchi za visiwani.

Amesema hali hiyo sio ya Zanzibar tu bali dunia nzima lakini Zanzibar iliathiri zaidi kutokana na utegemezi wake katika sekta ya utalii.

“Katika kipindi cha 2020 kasi ya ukuaji wa uchumi Zanzibar iliporomoka hadi asilimia 1.3 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya mwaka 2019 kabla ya kuingia kwa uviko 19, kwa upande wa utalii, idadi ya watalii walipungua 260,000 kutoka 538,000 mwaka 2019. Takwimu zinaonyesha asilimia 95 ya hotel zilizoko Zanzibar za kuanzia nyota moja zilifungwa au kupunguza shughuli zake na kupunguza wafanyakazi kwa zaidi ya asilimia 90,” amesema Rais Mwinyi

Amesema kwa Zanzibar maendeleo ya sekta ya utalii yamefungamana na maendeleo ya sekta nyingine hivyo kuanguka kwa utalii na kufungwa kwa hoteli kuliathiri sekta ya kilimo, uvuvi, ufugaji, usafirishaji, biashara na ujasiriamali hatua iliyopunguza mzunguko wa fedha.

Watu 11 wafariki Dunia kwenye Show ya Travis Scott.
Kibali chatolewa kukamatwa kwa aliyekuwa Rais