Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema moja ya tatizo kubwa walionalo watumishi wa serikali ni uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Amesema hayo kupitia Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter leo Julai 8, 2021 ambapo ameandika kuwa kwa kile kilichojiri mara baada ya baadhi ya watumishi wa serikali kusikia juu ya ziara yake katika eneo la Welezo, wahusika kutatua tatizo la wananchi.
“Tatizo kubwa la watumishi Serikalini ni uwajibikaji, nimesikia maji yameanza kutoka baada ya kusikia nakuja hapa Welezo,” amesema Rais Dkt. Mwinyi.
Rais Dkt. Mwinyi anafanya ziara ya wiki moja katika mikoa mitatu ya Unguja kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo leo hii anafanya ziara katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Welezo.
Aidha Dkt. Mwinyi ametoa agizo kwa watendaji wote wa Serikalini kwa upande wa elimu, afya, barabara na maji waje na mpango wa kudumu kwa kipindi cha mwezi mmoja.