Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi kujiandaa na sense ya watu na makazi itakayofanyika agost 2022.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 8,2021 Mkoani Morogoro alipohudhuria Mkutano Mkuu wa Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT).

Amewataka wananchi kuachana na imani na dhana potofu zinazojengwa miongoni mwao kwani lengo la sensa ni kupata idadi kamili ya Watanzania tofauti na hivi sasa ambapo kuna makadirio tu.

Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa zoezi la Sensa ndio litakalotoa dira katika kuweka malengo na kuandaa mipango ya maendeleo.

Waziri Mkumbo azindua Bodi ya wakurugenzi TBS
Rais Mwinyi: Uwajibikaji ni tatizo kwa watumishi wa Serikali