Waziri wa Viwanda na Biashara Kitila Mkumbo amewataka Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania TBS kuongeza tija na thamani katika kutatua changamoto za msingi na kuhakikisha TBS inaendelea kuwa kwenye ubora wake.

Ameyasema hayo leo Julai 8,2021 wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, ambapo amewasisitizia kutambua majukumu yao ili wasiingiliane na majukumu ya Menejimenti.

Aidha Waziri Mkumbo ameonya Bodi hiyo kwa kuwakumbusha kufanya majukumu yao katika kutatua changamoto na sio kujiona kama waajiriwa wa TBS wakati wao ni wajumbe wa Bodi, huku akisisitiza kushirikiana kwa pamoja ili kutimiza malengo ya Taasisi.

Amesema kuwa endapo Bodi itakuwa ni chanzo cha changamoto wataishauri serikali na kuivunja bodi hiyo, huku akisisitiza Bodi haiitaji mjumbe ambaye ni kikwazo katika kulipeleka shirika mbele zaidi.

Hali kadhalika Waziri Mkumbo ameikumbusha Bodi hiyo kuanza na viporo vilivyopo katika kutatua changamoto kwenye Taasisi ikiwemo pamoja na suala la ukaguzi wa magari bandarini na kuishauri manejimenti, lakini pia suala la wafanyabiashara wadogo kuona ni jinsi gani watatoa kwa urahisi alama za ubora kwa wafanyabiashara kwa kushirikiana na SIDO.

Naye Mwenyekiti wa Bodi Dkt Fenella Mukangara amehaidi kufanya kazi kwa bidii na kutatua changamoto zote na kuahidi kuwa msikivivu na kuishauri manenjimenti katika kujenga.

Simba Queens yaangukia Kundi A CECAFA
Tushiriki sensa tuendane na mipango ya maendeleo- Rais Samia