Serikali imezindua mradi wa kuboresha mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknololojia pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO. 

Wakati wa uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe amesema kwa kutambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu kwa sasa serikali i[po kwenye mchakato wa kuandaa sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kwamba Wizara iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukamilisha uandaaji wa sera hiyo. 

Amesema kuwa mpaka sasa hakuna sera ya sayansi , teknolojia na ubunifu zaidi ya kuwa na sera ya sayansi ilitungwa mwaka 1996 ambayo ndio inatumika kwa sasa. 

Awali akitambulisha mradi huo Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia kutoka UNESCO Keven Robert amesema kuwa mradi huo utawezesha kusaidia nchi kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na utafiti.

Mradi huo pia utasaidia kuimarisha taasisi za kisayansi kufanya tafiti na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti za kisayansi ambazo zitasaidia katika kutatua changamoto za wananchi, kukabiliana na majanga yakiwemo magonjwa mbalimbali na pia kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Robert amesema kuwa mradi huo utakuwa na maeneo10 ya utekelezaji ambapo baadhi ya maeneo ni pamoja na kuangalia uwekezaji katika tafiti za kisayansi ambapo matokeo ya tafiti hizo zinapouzwa zinaweza kuimarisha uchumi ya nchi.

Zulu aahidi makubwa Azam FC
KMC FC yaitambia Simba SC