Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako, ametoa wito kwa wabunifu kuwasiliana na COSTECH kupitia mitandao ya kijamii ama kufika katika ofisi zao ili ubunifu wao utambuliwe na kuweza kusaidiwa kupitia kambi za wabunifu ambazo ziko chini yao.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea banda la COSTECH katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa.

Aidha Waziri Ndalichako amesema kuwa COSTECH imekuwa ikiendeleza wabunifu kila mwaka kumekuwa na mashindano ya bunifu MAKISATU yakisimamiwa na costech abayo yanasaidia kuendeleza bunifu za watu mbalimbali nchini.

“Nimefurahi kuona kwamba zile nadharia ambazo zinafundishwa zinaenda mbali wanaweza kufanya vitu kwa vitendo ambavyo moja kwa moja vinaenda kugusa katika kujenga ujuzi unaomwezesha mtu kujiajiri au kuajiriwa katika sekta ambazo zinagusa changamoto za Watanzania,” Amesema Prof.Ndalichako.

Hata hivyo Profesa Ndalichako ameahidi kushilikiana na Wizara ya Viwanda na biashara kuhakikisha wanawasaidia wabunifu kutafuta soko kutokana na bunifu zao.

“Katika ubunifu nyingi ambazo nimeziona zinalenga katika kutatua matatizo ya kijamii kwahiyo nitoe wito kama kuna changamoto ya kimasoko pia nalo tutashirikaiana na Wizara ya Viwanda na Biashara tuone ni namna gani tunaweza kuwasaidia kuwatangaza zaidi ili waweze kupata wateja wengi na biashara zao au ubunifu wao uweze kwenda kutoa mchango kwenye taifa letu,” Amesema Prof.Ndalichako.

Sambamba na hayo yote Tume ya Sayansi na Teknolojia imeshika nafasi ya pili katika maonesho ya mwaka huu ya 45.

KMC FC yaitambia Simba SC
Mzee Mpili: Simba SC atapigwa Kigoma