Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kuwa kiongozi wa kudumu ndani ya chama hicho ambaye anaweza kutawala milele.
Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye alikozaliwa Rais Nkurunzinza Kaskazini mwa nchi hiyo.
Aidha, uamuzi huo umechukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.
Hata hivyo, Wanaharakati wa siasa nchini Burundi wanasema kuwa hatua hiyo imezamilia kuua mjadala wa nani atakayemrithi rais katika uchaguzi wa mwaka 2020.